Waislamu duniani kote wanaendelea kumzuru Imam Hussein (AS) na kufuata Njia yake ya kupigania Haki na Ukweli. Katika majlisi hizi, waumini huomba dua kwa Mwenyezi Mungu awaondolee shida, maradhi na dhiki, na awafungulie milango ya riziki na baraka.

15 Agosti 2025 - 17:10

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Leo hii (15-08-2025), Waislamu Duniani kote wanaadhimisha siku 40 tangu kuuawa kishahidi kwa Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), Imam Hussein (as), katika tukio tukufu la Karbala.

Ziara ya Arubaini: Sahaba wa Mtume (s.a.w.w) Jabir bin Abdillah Al-Ansar na Kumbukumbu ya Mashahidi wa Karbala + Picha

Imam Hussein (AS) aliuwawa kikatili na maadui wa Uislamu, mwili wake ukapondwa na kukanyagwa na farasi wa maadui hao, bila heshima ya jeneza kama ilivyo desturi kwa wafu. Tukio la Karbala lilikuwa siyo vita ya kisiasa tu, bali ni mapambano ya kudumu baina ya Haki na Batili, yaliyobeba ujumbe wa kudumu kwa vizazi vyote.

Ziara ya Arubaini: Sahaba wa Mtume (s.a.w.w) Jabir bin Abdillah Al-Ansar na Kumbukumbu ya Mashahidi wa Karbala + Picha

Kumlilia na kumkumbuka Imam Hussein (AS) ni kumheshimu na kumhuisha Mtume Muhammad (SAWW), kwani Mtume mwenyewe alisema: 

"Hussein -as- anatokana na Mimi, na Mimi ninatokana na Hussein."

Wapenzi wa Mtume (SAWW) daima humzuru na kumkumbuka Imam Hussein (AS) hasa katika Ziara ya Arubaini. Mzuru wa kwanza wa Imam Hussein (AS) baada ya mauaji ya Karbala alikuwa Sahaba maarufu wa Mtume, Jabir bin Abdillah Al-Ansar. Jabir alimtembelea Imam Hussein (AS) siku ya 40 tangu kuuawa kwake (Arubaini), akamzuru kwenye kaburi lake na pia kuwatembelea mashahidi wengine wa Karbala.

Jabir alisema katika ziara yake:

"Natamani ningelikuwa pamoja nanyi, na nikafuzu pamoja nanyi kufuzu kukubwa."

Katika ziara hiyo, Imam Zainul-Abidina (AS) aliwasili Karbala akiwa na msafara wake na kukutana na Jabir. Imam alimweleza Jabir matukio yote ya Karbala, akimwonyesha sehemu ambapo muovu Shimr bin Dhil Jaushen alimkalia kifuani Imam Hussein (AS) na kumkata kichwa.

Ziara ya Arubaini: Sahaba wa Mtume (s.a.w.w) Jabir bin Abdillah Al-Ansar na Kumbukumbu ya Mashahidi wa Karbala + Picha

Katika siku hiyo ya kumbukumbu, Imam Zainul-Abidina (AS) alifanya tukio muhimu la kuunganisha kichwa na kiwiliwili cha Imam Hussein (AS), ambavyo vilikuwa vimezikwa tofauti, na kuvihifadhi kwenye kaburi moja.

Waislamu duniani kote wanaendelea kumzuru Imam Hussein (AS) na kufuata Njia yake ya kupigania Haki na Ukweli. Katika majlisi hizi, waumini huomba dua kwa Mwenyezi Mungu awaondolee shida, maradhi na dhiki, na awafungulie milango ya riziki na baraka.

Your Comment

You are replying to: .
captcha